Kipa Yaw Berko raia wa Ghana, amemuambia
Kocha wake, Zdravko Logarusic kwamba akimpa nafasi naye ataonyesha uwezo.
Kocha huyo raia wa Serbia alisema jana
ataanza kumpa nafasi Berko katika mechi ya leo ya michuano ya Mapinduzi dhidi
ya KMKM.
“Kama nitapata nafasi litakuwa jambo
zuri, nitaifanyia kazi na kocha akiwa kwenye benchi naamini atafurahi,” alisema
Berko.
Logarusic amekuwa akimtumia kipa Ivo
Mapunda ambaye aliwahi kufanya naye kazi kwenye kikosi cha Gor Mahia ya Kenya.
Berko ameingia mkataba wa miezi sita
kuidakia Simba na baada ya msimu huu atalazimika kuondoka kwa kuwa TFF
imepitisha sheria ya wachezaji watatu wa kimataifa lakini hakuna golikipa.
0 COMMENTS:
Post a Comment