Winga mwenye kasi wa Simba, Ramadhani
Singano ‘Messi’ amesema hawezi kuvimba kichwa kutokana na mafanikio
anayoyapata.
Akizungumza na SALEHJEMBE, Messi alisema
yeye ni mtu anayejali mafanikio lakini anathamini mchango wa watu.
“Ninaishi na watu na ndiyo wanaonisaidia
kuendelea, hivyo siwezi kuwa na dharau.
“Lakini kitu kizuri lazima nao waamini
mimi ni mwanadamu, ikitokea nimekosea basi wanielewe,” alisema.
Messi amekuwa gumzo kutokana na uwezo
ambao amekuwa akiuonyesha katika mechi mbalimbali.
Katika michuano ya Mapinduzi
inayoendelea mjini Zanzibar, Messi amekuwa kati ya wachezaji gumzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment