BOBAN (WA TATU KUSHOTO) AKIWA NA WACHEZAJI WENZAKE WA COASTAL UNION KWENYE MSTARI WA KUINGIA NDANI YA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA JULIUS NYERERE. |
Kiungo wa Wagosi wa Kaya, Coastal Union,
Haruna Moshi ‘Boban’ ameondoka leo na kikosi hicho kwenda kwenda Oman kuweka
kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Boban alikuwa katika muonekano tofauti
kabisa na ilivyokuwa awali baada ya kunyoa rasta zake.
Kawaida Boban amekuwa akionekana na
rasta hizo, lakini leo ilikuwa tofauti kabisa.
Hali hiyo ilisababisha mashabiki
waliokuwa uwajani hapo kushindwa kumtambua huku wengine wakidhani hakuwa kwenye
msafara huo.
Coastal Union wameondoka leo mchana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar wakiwa na
kikosi chao kamili.
0 COMMENTS:
Post a Comment