Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema sasa yuko katika wakati mzuri kuanza kuwasuka washambuliaji.
Logarusic amesema amekuwa katika wakati
wa kuwasuka mabeki kuhakikisha anakuwa na safu imara ya ulinzi.
“Lakini sasa naweza kufanya kazi ya
viungo na washambuliaji kwa kuwa tayari nina imani na safu ya ulinzi,” alisema.
Logarusic alisema ana imani baada ya
muda mfupi, safu yake ya ulinzi itaanza kuwa tishio kwa kuwa ina washambuliaji
wazuri lakini wanahitaji mafunzo.
0 COMMENTS:
Post a Comment