Timu ya Mbeya City juzi ilitua kisiwani
Zanzibar kwa makundi mawili ikionyesha mkwara mzito kwa kutumia shirika la
ndege la ZanAir na moja kwa moja wakaenda Gombani kwa ajili ya mazoezi.
Timu hiyo ambayo ni gumzo kwa sasa
ilitua Zanzibar majira ya jioni ikiwa na wachezaji 20 pamoja na viongozi watano
huku kocha mkuu, Juma Mwambusi akisema hawakwenda Zanzibar kutembea bali
kufanya kazi.
Alisema pamoja na kwamba walifanya
vizuri kwenye ligi kuu, wanaamini kuwa watakutana na upinzani mkubwa kwenye
michuano hiyo hivyo wamejiandaa vyema kufanya makubwa.
“Timu za Zanzibar zimekuwa zikisumbua sana
timu za Tanzania Bara, ila sisi tumekuja kutoa upinzani mkali kwa timu hizo,
licha ya kuwa wageni katika michuano hii, ukweli hatukuja huku kutalii,”alisema
Mwambusi.
Aidha alikishukuru chama cha soka
Zanzibar kwa kuwapatia nafasi katika kushiriki katika michuano hiyo.
Alisema kuwa wachezaji wake wamekuwa na
habari kubwa sana juu ya michuano hiyo kwa lengo la kuwaonyesha wapenzi wao na
mashabiki kile ambacho waliweza kuvionyesha vigogo vya ligi kuu ya Tanzania Bara
katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment