Uongozi wa Klabu ya Simba umesema
utamuongeza mkataba kocha wao, Zdravko Logarusic, mara baada ya kumalizika kwa
michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Loga aliyejiunga na Simba kwenye dirisha
dogo akichukua mikoba ya Abdallah Kibadeni na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, amesaini
mkataba wa miezi sita.
Mmoja wa
mabosi wa Simba ambaye hakutaka kutajwa jina alisema kuwa wameridhishwa na
kiwango cha timu yao kilichoonyeshwa kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe, hivyo
muda wowote mara baada ya kumaliza michuano ya Mapinduzi watamsainisha.
Alisema wamesikia fununu za kocha huyo
kuwindwa pia na mahasimu wao, Yanga, lakini hiyo haiwatishi kwa kuwa wanajua
wanataka kuwaharibu kisaikolojia hivyo wametambua janja yao na hawana hofu.
“Tumefurahishwa na kiwango cha timu
walichokionyesha kwenye mechi ya Mtani, hivyo tunafikiria kumuongeza mkataba
mara baada ya Mapinduzi.
“Tumesikia fununu za Yanga kumtaka Loga lakini
ukweli hazitutishi kwani tunaamini ni kocha wetu ambaye tunaelewana naye
vyema,” alisema.
Ingawa ni kimyakimya lakini watani wao Yanga wamekuwa na mpango wa kutaka kumyakua kocha huyo raia wa Croatia kwa ajili ya kukinoa kikosi chao kilichokuwa kikinolewa na Ernie Brandts.
0 COMMENTS:
Post a Comment