Kiungo Athumani Iddi ‘Chuji’ amerejeshwa
kundini na kufanikiwa kujiunga na wenzake wanaojiandaa na mechi dhidi ya Mbeya
City.
Chuji amejiunga na Yanga ambayo imeweka
kambi mjini Bagamoyo baada ya mchezo wake dhidi ya Coastal Union mjini Tanga
uliomalizika kwa sare ya bao 1-1.
Mkongwe huyo katika kugawa mipira,
aliomba radhi kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wenzake kwamba
kitendo alichokifanya hakikuwa sahihi.
Chuji alisimamishwa kwa mda usiojulikana
kutoana na utovu wa nidhamu na SALEHJEMBE ilikuwa ya kwanza kuanika kwamba
kusimamishwa kwake kulitokana naye kuondoka wakati kikosi kikiwa uwanjani
kinapambana katika mechi ya Nani Mtani Jembe.
Kiungo huyo mwenye uwezo wa kupiga pasi
za mbali zinazofika kuliko mwingine yoyote nchini, atakuwa amekutana kwa mara
ya kwanza leo na Kocha Mkuu, Hans van Der Pluijm ambaye amejiunga na Yanga
wakati yeye akiwa kifungoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment