Azam imeweka rekodi kuwa klabu ya kwanza
nchini ambao uwanja wake utatumika katika michuano iliyo chini ya Shirikisho la
Soka la Kimataifa, Afrika.
Azam FC imeweka rekodi hiyo baada ya Caf
kuupitisha uwanja wake kutumika katika michuano ya Kombe la Shirikisho.
Azam itaanza kazi na Ferreviario ya
Msumbuji na ililazimika kufanya ukarabati wa nguvu ili kufikia viwango
vinavyotakiwa
Mkurugenzi wa mashindano wa Caf, Khaled
Naser amethibitisha kuhusiana na hilo na sasa unakuwa uwanja wa kwanza wa klabu
kutumika chini ya Caf.
Kabla ya hapo, klabu zote zikiwemo
Simba, Yanga, Mtibwa Sugar, Pamba ya Mwanza na nyingine zilizowahi kushiriki
michuano ya Caf zimekuwa zikitumia viwanja vya CCM au vile vya serikali.
0 COMMENTS:
Post a Comment