Wagosi wa Kaya, Coastal Union wameondoka
leo kwenda Oman kuweka kambi kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Coastal Union wameondoka leo mchana
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar wakiwa na
kikosi chao kamili.
Kivutio zaidi ilikuwa ni namna baadhi ya
matenga ya nyanya ambayo walibeba uwanjani hapo.
Haikujulikana mara moja kama Coastal
watakuwa wakipiga wenyewe watakapokuwa jijini Muscat au ni zawadi.
Lakini wachezaji wake walionekana kuwa
fiti na tayari kwa ajili ya kambi hiyo nchini Oman.
0 COMMENTS:
Post a Comment