VOGTS AKIWA NA MKWASA KWENYE MAZOEZI YA YANGA. |
Wachezaji
wa zamani wa timu ya Taifa ya Ujerumani ambao kwa sasa ni makocha wa timu
ya Taifa ya Azerbeijan Berti Vogts na msaidizi wake Wolfgang leo jioni kabla ya
mazoezi waliibuka katika viwanja vya hotel ya Sueno Beach na kuongea kidogo na
makocha wa Young Africans Hans na Mkwasa masuala ya kiufundi kisha kuagana nao
na kuwaacha waendelee na progam yao ya mazoezi.
Vogts amabaye alikuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa Ujerumani kwa
miaka nane (1990-1998) na kufanikiwa kushinda kombe la Ulaya mwaka 1996, na
kufika hatua ya robo fainali ya kombe la Dunia mwaka 1998 alikuwa ameambatana
na kocha wake msaidizi Wolfagang .
MKWASA AKIWA NA WOLFGANGA |
Kocha mpya wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Pluijm leo
ameanza rasmi kazi ya kukinoa kikosi cha mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania
bara katika viwanja vya hoteli ya Sueno Beach Side baada ya jana kuiongoza
katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Altay SK.
Hans ambaye amejiunga na Young Africans wiki hii akichukua nafasi
ya kocha mholanzi aliyeondoka Ernie Brandts amesema atajitahid kadri ya uwezo
wake pamoja na wachezaji na benchi la ufundi kuona wanaisaidia timu kufika
hatua nyingine mbele zaidi.
"Amesema hawezi kufanya jambo lolote peke yake bali kwa
kushirikiana kwa pamoja atafanikiwa kwani katika mchezo wa jana timu yake
iliweza kucheza soka la kujituma na kushirikiana mwanzo mwisho kitu ambacho
ndio falsafa yake katika ufundishaji" alisema van Der Pluijm.
MKWASA NA BOSI WAKE, VAN DER PLUIJM |
Timu ilifanya mazoezi ya asubuhi leo saa 5 kamili kwa saa za
Uturuki mpaka saa 6:30 kabla ya kupumzika na kurejea tena mazoezini jioni saa
11 kamili jioni mpaka saa 12:30 ambapo alikuwa akiwaelekeza wachezaji jinsi
gani anapendelea wacheze kwa kufuata mfumo wake.
Akizungumza baada ya mazoezi ya leo asubuhi, Kocha van Der Pluijm amesema
timu ya Young Africans ina wachezaji wazuri ambao wana uwezo binafsi na bado
wana nafasi ya kucheza soka kwa kipindi kirefu hivyo kikubwa wanapaswa kuwa fit
muda wote ili waweze kutimiza majukumu yao.
Young Africans itaendela na mazoezi kesho na asubuhi katika
viwanja vya hotel ya Sueno kujiweka sawa kwa mchezo utakaofuata wa kirafiki
kabla ya kurejea nchini wik ijayo tayari kwa mikikiki ya Ligi Kuu ya Vodacom na
mashindano ya kimataifa.
SOURCE: www.youngafricans.co.tz
0 COMMENTS:
Post a Comment