Kocha Mbelgiji, Luc Eymael akimuomba
radhi akimtaka asiamini kwamba yeye amembeza Hans van Der Pluijm.
Katika barua pepe ya kocha hiyo ambayo
Championi Ijumaa limeishuhudia na kopi linayo, van Der Pluijm amemuomba radhi
pia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah Bin Kleb.
“Mimi ni kocha ninayejali taalum yangu,
ninafuata weledi, hata kidogo siwezi kuzungumzia na kumponda kocha mwingine,
kuna gazeti la hapo Tanzania limeandika ambacho sikusema na mwandishi
amenilisha maneno.
“Tafadhari, namba niseme hivi, naomba
radhi kwa kilichoripotiwa kwenye chombo hicho cha habari cha Tanzania kwamba
ninasema mtafungwa na Simba milele, kitu ambacho hakiwezekani kwenye mpira,”
aliandika kwenye barua pepe hiyo.
Lakini alipoulizwa na gazeti hili sababu
za kuomba radhi kwa uongozi wa Yanga wakati yeye si kocha wa kikosi hicho,
Eymael aliyewahi kuwa kocha wa AFC Leopards alisema:
“Uungwana ni kitu kizuri sana, nashangaa
kilichoandikwa kwa kuwa si lahisi kocha mwenye akili timamu amponde mwenzake
bila ya sababu. Sijawahi kuziona Yanga au Simba zikicheza, lakini Yanga si adui
zangu, lazima niwaombe radhi.
“Najisikia vibaya kwa kuwa walioandika
wametaka kunitegenezea maadui Tanzania bila ya sababu, nimesema vitu tofauti
kabisa. Nimekasirika sana na siku yangu si nzuri tena, leo.
“Kama Yanga watanielewa, litakuwa jambo
zuri kwa kuwa nimetumia uungwana. Lakini isipokuwa hivyo nitasikitika sana.”








0 COMMENTS:
Post a Comment