Na Baraka Kizuguto, Antalya
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania timu ya Young Africans jana imetoka sare ya
kutokufungana (0-0) dhidi ya timu ya KS Flamurtari inayoshiriki Ligi Kuu nchini
Albania katika mchezo uliofanyika usiku wa leo katika viwanja vya Side Stars
Complex Manavgat Antalya
Ukiwa
ni mchezo wake tatu tangu iweke kambi nchini Uturuki, Young Africans mpaka sasa
imeshashinda michezo miwili dhidi ya Ankara Sekerspor 3-0, Altay SK 2-0 kabla
ya kutoka sare leo.
Kocha
Mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van Der Plyum leo alikua akikikiongoza
kikosi chake kwa mara ya pili baada ya kukiongoza katika mchezo wa awali dhidi
ya Altay SK.
Akiongelea
mchezo wa leo kocha Hans amesema vijana wake wamecheza vizuri, timu zote ziliweza
kucheza kwa nafasi, lakini kwa umakini wa walinzi wa timu zote ndio maana
milango ilikua migumu kufunguka.
KS
Flamurtari ni timu nzuri, awali hawakutegemea kama watapata ushindani mkali
kutoka kwetu, lakini kadri mchezo ulivyokua ukiendelea walishangaa kuona tuna
kikosi safi kilichokamilika.
“Washambulaji
wetu walipata walipata nafasi kadhaa lakini hawakuweza kuzitumia
vizuri, hali kadhalika mlinda mlango wetu Dida aliweza kuokoa hatari nyingi
kipindi cha pili kutoka kwa wapinzani wetu” alisema Hans.
Young
Africans imebakisha siku tano kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini Tanzania
tayari kwa mikikimiki ya Ligi Kuu ya Vodacom na Mashindano ya kimataifa.
Young Africans:
1.Deogratias
Munishi “Dida”, 2.Juma Abdul, 3.David Luhende, 4.Mbuyu Twite, 5. Kelvin
Yondani, 6.Frank Domayo, 7.Mrisho Ngasa/Said Bahanuzi, 8.Haruna Niyonzima,
9.Didier Kavumbagu/Saimon Msuva, 10.Emmanuel Okwi, 11.Hamis Kiiza
0 COMMENTS:
Post a Comment