January 19, 2014





Uongozi Yanga umelia kuzushiwa kwamba timu hiyo imepigwa mabao 7-1 katika moja ya mechi za kirafiki nchini Antalya, Uturuki.
 
Ingawa Ofisa Habari wake, Baraka Kizuguto hakuweka mambo wazi, lakini kwenye Facebook ya klabu hiyo ameeleza kwamba kuna watu wanalazimisha rangi ya bluu kuwa njano.
Kuna taarifa zimezagaa kwamba Yanga imechapwa mabao hayo saba lakini watu wakaambia "wakaushe".

Kizuguto aliweka hivi kwenye Facebook:

Zinatumika nguvu nyingi kubadilisha Bluu kuwa Njano, ila ukweli utabakia vile vile:

Young Africans Sports Club tangu iweke kambi nchini Uturuki imeshacheza jumla yamichezo mitatu tu ya kirafiki ya kujipima nguvu, na mpaka sasa na matokeo ni kama ni ifuatavyo:

11.01.2014 - Side Crown Venue:
Ankara Skerspor 0 - 3 Young Africans (Didier, Okwi, Kiiza)

15.01.2014 - Suneo Beach Hotel:
Altay SK 0 - 2 Young Africans (Didier, Okwi)

18.01.2014 Side Stars Complex:
KS Flumartari 0- 0 Young Africans

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic