KIBADENI (WA KWANZA KUSHOTO) WAKATI AKIWA KAZINI SIMBA, WANAOMFUATIA NI JULIO, NICO NYAGAWA NA DAKTARI WA TIMU. |
Kocha Mkuu wa Ashanti United,
Abdallah Kibadeni, amewamwagia sifa viongozi wa timu hiyo kwa kusema kuwa
wanafanya kazi kwa kuzingatia utaratibu na mipaka ya kiutendaji, tofauti na
alivyokuwa Simba.
Kibadeni alisema hivi sasa anafanya
kazi yake kwa amani zaidi bila ya presha na amepewa mamlaka makubwa zaidi na
viongozi wa klabu hiyo.
Alisema hali hiyo itamfanya atekeleze
mikakati yake ya maendeleo aliyojiwekea kwa utulivu zaidi ili timu hiyo iweze
kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara utakaoanza Januari 25.
“Sina wasiwasi kwani hivi sasa
nimetulia na ninafanya kazi yangu kwa amani zaidi bila presha ukilinganisha na
nilivyokuwa Simba.
“Viongozi wa Ashanti United kila
mmoja anafanya kazi yake kwa kufuata utaratibu, jambo ambalo sikuwahi kuliona
katika timu nyingine ya ligi kuu,” alisema Kibadeni ambaye kabla ya kuinoa
Simba alikuwa kocha wa Kagera Sugar.
0 COMMENTS:
Post a Comment