Vita ya kuwania ufungaji bora wa Ligi
Kuu Bara imenoga, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast amefikisha mabao 10 sawa
na mshambuliaji wa Simba, Amissi Tambwe.
Tambwe raia wa Burundi alianza na kasi
kubwa katika mzunguko wa kwanza, lakini hadi mzunguko wa kwanza unamalizika
alikuwa na mabao hayo kumi.
Katika mechi ya kwanza ya Simba ya
mzunguko wa pili wa ligi hiyo dhidi ya Rhino, Tambwe alitikisa nyavu mara
mbili, lakini mara moja akawa ameotea na mara ya pili akamsukuma beki wa Rhino
, hivyo kubaki na mabao yake 10.
Leo, Tchetche amefunga bao pekee la Azam
FC katika mechi dhidi ya Rhino na kufikisha mabao hayo 10 za Mrundi huyo, hali
inayoonyesha vita ya ufungaji mabao ndiyo kwanza kumekucha.
0 COMMENTS:
Post a Comment