Azam FC imeonyesha kama wakizubaa, basi
inabeba ubingwa baada ya kuichapa Rhino ya Tabora kwa bao 1-0 na kupaa kileleni mwa ligi.
Kwa ushindi huo, Azam FC imesikisha
pointi 33 na kuiteremsha Yanga yenye pointi 32 ambayo ilikuwa inaongoza hadi
mwishoni mwa mzunguko wa kwanza.
Kabla ya kushuka uwanjani leo mjini Tanga, Yanga ilikuwa na pointi 31, pointi moja zaidi ya Azam FC, lakini sare dhidi ya Coastal imeifanya ishike nafasi ya pili.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye
Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Mbagala jijini Dar, bao pekee la mchezo huo
lilifungwa na Kipre Herman Tchetche raia wa Ivory Coast.
Azam inayofundishwa na Kocha Omog raia
wa Cameroon ilionyesha soka la taratibu lakini pasi za taratibu na uhakika na
mwisho ikafanikiwa kushinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment