Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic
amefunga safari kwenda kuiona Azam FC leo ikivaana na Spices katika mechi ya
Kombe la Mapinduzi.
Logarusic ameiambia SALEHJEMBE kwamba
amefanya hivyo kwa kuwa hajapata nafasi ya kuiona Azam FC ikicheza.
“Niliiona Yanga halafu nikaiona kwa mara
ya pili wakati tukicheza nayo. Lakini sijawahi kuiona Azam FC,” alisema.
“Kwa kuwa ni wapinzani wetu kwenye ligi,
ni lazima kuona wakicheza na kujifunza mambo kadhaa,” alisema.
Simba na Azam FC, kila moja imeanza
mechi yake ya kwanza kwa kushinda.
0 COMMENTS:
Post a Comment