MKWASA KAZINI SIKU YA KWANZA |
Kocha Msaidizi wa Yanga, Boniface
Mkwasa, amewataka wachezaji wake kuamini kazi imeanza.
Mkwasa ametaka kila mchezaji wa Yanga
kujituma na kuamini wamerudi kazini.
“Baada ya mabadiliko, makocha kuondolewa
utaona mambo yaliyumba. Lakini sasa tumeanza kazi na kila mmoja arudishe akili
yake.
“Suala la tutaweka kambi wapi
tunaliachia kwa uongozi lakini sisi ni kuongeza juhudi na umakini katika
mazoezi,” alisema.
Mkwasa alianza kazi Yanga rasmi jana
kwenye Uwanja wa Bora Kijitonyama jijini Dar.
Kabla ya kutua Yanga, Mkwasa ambaye si
mara ya kwanza kuifundisha timu hiyo alikuwa akiinoa Ruvu Shooting.
wafanye juhudi mana ndo wawakilishi wetu kwa mashindano ya mabingwa wa africa
ReplyDelete