Mshambuliaji nyota Robert
Lewandowski ameamua kumuajiri mlinzi maalum wa kumlinda dhidi ya mashabiki wa
timu yake ya zamani ya Borussia Dortmund.
Mshambuliaji huyo amekuwa
adui wa mashabiki wa Dortimund baada ya kujiunga na wapinzani wao Bayern
Munich.
Kutokana na maneno ya hasira
kutoka kwa mashabiki hao na siku zinasonga kabla ya timu hizo kukutana,
mshambuliaji huyo amesisitiza atakodi mlinzi.
Taarifa zinaeleza kuwa Lewandowski ameonywa kuwa na uhakika na sehemu
anazotembelea hasa kipindi hiki mashabiki hao wa BVB wakiwa bado na hasira
kutokana na kuhama kwake.
0 COMMENTS:
Post a Comment