January 25, 2014


MPIRA UMEKWISHA:

Dk 90, kushambuliana kwa zamu, Javu anakosa bao baada ya mpira wake wa kichwa kushindwa kulenga



Dak ya 80, Javu anaingia kuchukua nafasi ya Kavumbagu.
GOOOOOOOO Dk 79, Luhende anaifungia Yanga bao baada ya kuwatoka mabeki wa Ashanti na kupiga krosi ya chini lakini kipa anausindikiza mwenyewe mpira wavuni

 Dk 69, Ashanti inafanya mabadiliko, anaingia Idd Silas kuchukua nafasi ya Mohammed Fakhi
Dk 64, Ashanti wanashambulia tena na kuonyesha kuwazidi sana Yanga, lakini Dida anaokoa shuti tena.


Dk 61, Sued anabaki na Dida, anajaribu kumpiga chenga lakini kipa anaokoa
GOOOOOO, Dk 59, Obina anaifungia Ashanti bao la kusawazisha baada ya Hussein Sued kufanya counter attack na kupiga krosi saafi iliyomkuta Mnigeria  huyo.


Dk 56, Kavumbagu yeye na kipa baada ya krosi ya Ngassa kumfikia, anashindwa kuunganisha.

Dk 54, Mtiro anapiga anachonga mpira wa faulo, unatoka juu la lango la Yanga
GOOOOOO Dk 50, Kavumbagu anamalizia kwa ulahisi wavuni baada ya Msuva kumtoa beki na kipa wa Ashanti.


Dk 46, Dida anafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la Sued na inakuwa Suad
MAPUMZIKO:
Dk 45+2, Niyonzima anawapiga chenga mabeki wa Ashanti na kupiga shuti kali lakini shuti linapita juu kidogo.


Dk 45, Sued anashindwa kuuwahi mpira na kufunga, Dida anaudaka

Dk 35, Yanga wanamtoa Bahanuzi anaingia Simon Msuva
Dk 21, Astanti wanasizi kuongeza mashambulizi na kuwapa Yanga wakati mgumu huku krosi za Sued zikikosa mfungaji.


DK 14, Ashanti wanashambulia na nusura Fakhi afunge lakini anashindwa kujiamini
Dk ya 11, Kavumbagu yeye na kipa, lakini anakosa baada ya kujaribu kumpiga kipa chenga.


Dk ya 9, Ashanti wanakosa bao baada ya kufanya shambulizi kali lakini Hussein Mahundi anashindwa kumalizia
Dk ya 7, Kavumbagu anashindwa kufunga hatua mbili kutoka langoni baada ya Luhende kuwatoka mabeki wa AShanti.
Dk ya 5, Dida anachichanganya na Twite lakini Obina anashindwa kuuwahi na kufunga.


Dk ya 2, Ngassa anashindwa kufunga akiwa ndania ya hatua nane kutoka lango la Ashanti.

VIKOSI:


ASHANTI:-
Masognwe,Mkongo, Abdul Mtiro, Shaffi Hassan, Tumba Sued, Mohammed Fakhi, Abdul Manani, Fakhi Hakika, Bright Obina, Hussein Sued na Joseph Mahundi
YANGA:- 
Dida, Juma Abdul, Joshua, Twite, Yondani, Domayo, Ngassa, Niyonzima, Bahanuzi, Kavumbagu na Joshua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic