January 25, 2014

VAN DER PLUIJM AKIWA NA BAADHI YA WACHEZAJI WA YANGA WALIPOKUWA KAMBINI NCHINI UTURUKI.

Kocha Mkuu wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema watacheza mechi ya leo kwa kasi kubwa.

Yanga inashuka dimbani leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar kucheza na Ashanti United katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mechi hiyo itakuwa ya kwanza ya mashindano kwa kocha huyo kuingoza Yanga akiwa katika benchi. Awali aliiongoza katika mechi mbili za kirafiki nchini Uturuki ilikokuwa imeweka kambi na zote zilimalizika kwa sare.

Van Der Pluijm amesema pamoja na mipango, soka la kisasa linahitaji kasi na umakini.

“Nataka kucheza kwa kasi kubwa, tunajua kila timu iliyo katika ligi itakuwa ni bora.
“Mimi itakuwa ni mara yangu ya kwanza, lakini kama tunataka ushindi lazima tuwe makini, tutumie nafasi tutakazotengeneza lakini lazima tucheze kwa kasi ya juu,” alisema van Der Pluijm.

Kuhusiana na kikosi chake, van Der Pluijm alisema baada ya mechi, ataweza kujibu maswali mengi zaidi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic