January 27, 2014


 Juan Mata amekabidhiwa jezi namba nane katika kikosi cha Man United na kufanya mambo yaende tofauti na ilivyokusudiwa.


Awali wengi waliamini Mata atalamba jezi namba 7, lakini taarifa zinaeleza jezi hiyo imehifadhiwa kwa kuwa Man United, wanaamini ‘mwenyewe’ Cristiano Ronaldo atarejea na kuivaa tena, ingawa haijulikani ni siku gani.

Jezi namba 7 ilikuwa inavaliwa na Anderson raia wa Brazil ambaye Man United imempeleka kwa mkopo, Fiorentina ya Italia ili aboreshe kiwango chake.

Mara ametua Man United kwa kitita cha pauni milioni 37 akitokea Chelsea.

WAKALI WALIOWAHI KUVAA NAMBA SABA KWENYE KIKOSI CHA MAN UNITED NA KUPATA MAFANIKIO MAKUBWA AMBAO NI GEORGE BEST, CANTONA, BECKHAM NA RONALDO.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic