Nahodha wa Barcelona, Xavi amesherekea
mechi yake ya 700 akiwa na timu hiyo na kusema ataendelea kubaki Barca hadi
atakapostaafu.
Xavi amesema hadithi za kwamba
anakwenda New York nchini Marekani au anafuata mamilioni ya fedha nchini Qatar,
haziko kaika mawazo yake.
“Nataka kubaki hapa hadi
nitakapomaliza mkataba wangu,” alisema Xavi kabla ya mechi dhidi ya Malaga
ambayo ingekuwa ni ya 700 kwake akiwa na Barca.
Baada ya mechi hiyo, alisifia kiwango
walichokionyesha na kuibuka na ushindi wa mabao 3-0, lakini pia akasisitiza
kwamba watamheshimu rais wa Barcelona,
Rosell aliyeachia ngazi na kumtakia
kila la kheri.
0 COMMENTS:
Post a Comment