Na Boniface Wambura, TFF
Timu ya Taifa ya vijana wenye umri
chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) itacheza na Afrika Kusini katika mechi za
mchujo kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Afrika kwa umri huo
zitakazofanyika mwakani nchini Niger.
Serengeti Boys ambayo pamoja na nchi
nyingine 17 zimeingia moja kwa moja katika raundi ya pili itaanzia mechi hiyo
nyumbani kati ya Julai 18-20 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika
nchini Afrika Kusini kati ya Agosti 1-3 mwaka huu.
Ikifanikiwa kuitoa Afrika Kusini,
Serengeti Boys itacheza mechi ya raundi ya tatu na ya mwisho na mshindi wa
mechi kati ya Misri/Sudan vs Congo Brazzaville.
Nchi nyingine ambazo zimeingia moja
kwa moja raundi ya pili ni Afrika Kusini, Angola, Benin, Botswana, Burkina
Faso, Congo Brazzaville, Ethiopia, Gabon, Ghana, Ivory Coast, Mali, Morocco,
Nigeria, Rwanda, Senegal, Tunisia na Zambia.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) inatarajia kutangaza benchi la ufundi litakaloiongoza Serengeti Boys hivi
karibuni.
0 COMMENTS:
Post a Comment