Kamati mpya ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi, Februari 4 mwaka
huu inatimiza siku 100 tangu iingie madarakani katika uchaguzi uliofanyika
Oktoba 28 mwaka jana.
Hivyo, Rais Malinzi atazungumza na
waandishi wa habari Februari 7 mwaka huu kuelezea utekelezaji wa Ilani yake ya
uchaguzi. Muda na mahali utakapofanyika mkutano huo mtaarifiwa baadaye.
0 COMMENTS:
Post a Comment