Simba imeendelea na mazoezi leo kwenye Viwanja vya
Kawe jijini Dar.
Chini ya Kocha wake, Dravko Logarusic, Simba imefanya
mazoezi lakini zaidi ilikuwa ni kutumia mipira.
Kocha huyo kutoka Croatia naye aliweza kuonyesha ujuzi
wake na kufanya mashabiki wamshangilie.
Logarusic aliuchukua mpira na kupiga danadana huku
akionyesha ujuzi hali iliyowavutia mashabiki wengi.
Simba imerejea jijini Dar es Salaam ikitokea Zanzibar
ambako ilishiriki michuano ya Mapinduzi na kufikia hatua ya fainali na kupoteza
mchezo kwa bao 1-0 dhidi ya KCC ya Uganda.
0 COMMENTS:
Post a Comment