VAN DER PLUIJM AKIWA NA NGASSA, NIYONZIMA NA JOB. |
Kocha Mkuu mpya wa Yanga, Hans van Der Pluijm ameanza
kazi rasmi kukinoa kikosi cha timu hiyo asubuhi na jioni jana, lakini akasema
kweli kikosi chake kipo sawa.
Van Der Pluijm raia wa Uholanzi, amesema kikosi chake
kina wachezaji waliojitosheleza na kinahitaji marekebisho madogomadogo.
Mholanzi huyo alikishuhudia kwa mara ya kwanza kikosi
hicho kikiwa kazini jana na kufanikiwa kuishinda timu ya Altay inayoshiriki
Ligi Daraja la Pili Uturuki kwa mabao 2-0.
Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto amesema kocha huyo
amefurahishwa na uchezaji na umoja wa timu hiyo.
“Amesema hajawahi kuona wachezaji wanaocheza kwa
kushirikiana na morali ya hali ya juu kama wa Yanga.
“Amewapongeza sana na kutaka waendeleze ushirikiano
lakini kuna mambo ameahidi atayabadilisha,” alisema Kizuguto.
“Asubuhi mazoezi yalikuwa ya kupasha mwili tu kwa kuwa
tulikuwa na mechi jana, lakini jioni mazoezi yameendelea kama kawaida,”
alisema.
Yanga ipo kambini mjini Antalya na van Der Pluijm ameungana
na wachezaji hao juzi akitokea jijini Dar es Salaam kupitia Kigali, Rwanda.
0 COMMENTS:
Post a Comment