Mabingwa wa soka Tanzania, Yanga, wametua salama nchini Uturuki na watafikia
katika hoteli ya kifahari ya Sueno Hotels Beach katika Mji wa Antalya.
Safari hii Yanga wameonyesha jeuri ya fedha zaidi kwa kuwa watafikia
katika hoteli hiyo ya kifahari yenye uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 1000 kwa
wakati mmoja.
Hoteli hiyo ya kifahari inamiliki viwanja vinne vya soka, vikiwemo
vikubwa viwili. Lakini pia kuna viwanja vya tenisi na michezo mingine kama ya
kuteleza kwenye maji.
Ufukwe wake una viti 1000 kwa ajili ya wateja wanaotaka kujipumzisha
lakini kuna sehemu maalum kwa ajili ya kufanyia mazoezi.
Hoteli hiyo ya kifahari iko umbali wa kilomita tano kutoka maporomoko ya
Manavgat ambayo hutembelewa na watalii wengi.
Umbali hadi kwenye Mji wa Antalya ni kilometa 70, kwenda Uwanja wa Ndege
wa Antalya ni kilomita 60 lakini kuna sehemu mbalimbali za kitalii zilizo
karibu yake kama Perge, Termessos na Aspendos.
0 COMMENTS:
Post a Comment