Tiketi za elektronik zimeshindwa
kufungua milango ya elektronik kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kuzua
tafrani kubwa.
Kawaida mashabiki huzitumia tiketi hizo
kufungua mlango, lakini walipojaribu leo ilishindikana na kusababisha zogo kwa
waliokuwa wanataka kuingia uwanjani.
Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga
umefurika mashabiki kibao waliojitokeza kushuhudia mechi inayoendelea kati ya
wenyeji Coastal Union dhidi ya mabingwa Yanga.
Kutokana na hali hiyo ililazimu
utaratibu wa kawaida uanze kutumika kwa mashabiki kuingia na tiketi kuchanwa
kama kawaida, kitu ambacho hakikuwa kimepangwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment