Na Mwandishi Wetu, Tanga
Sare ya bila mabao ndiyo majibu ya
mchezo wa leo wa Ligi Kuu Bara kati ya wenyeji Coastal Union dhidi ya Yanga
kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.
Coastal iliyoweka kambi nchini Oman
kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na Yanga ikaweka kambi nchini
Uturuki, zimeshindwa kufungana huku kila upande ukishindwa kutimiza
ulichoahidi.
Kila upande ulionyesha kupania mechi
hiyo, lakini hakuna timu iliyopata bao ingawa kila upande ulipoteza nafasi za
kufunga.
Kipindi cha pili, Yanga ilipoteza
mwelekeo katika kiungo, Niyonzima na Domayo wakipoteana na kutoa nafasi kwa
Haruna Moshi ‘Boban’ na Crispine Odulla kutamba na kusababisha hatari kadhaa.
Ngassa pia alipata nafasi ya kuifungia
Yanga bao lakini akashindwa kuitumia nafasi hiyo na mwisho kukawa hakuna
mshindi.
0 COMMENTS:
Post a Comment