MWENYEKITI WA SASA WA TASWA, JUMA PINTO |
Na Walusanga Ndaki
UCHAGUZI mkuu wa Chama cha Waandishi wa
Habari za Michezo Tanzania (Taswa) unatarajiwa kufanyika Februari 16, mwaka huu
jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyotumwa na katibu mkuu wa
chama hicho imesema kuwa kikao cha viongozi wa Taswa kilichofanyika juzi kimeamua kuwa mkutano huo ufanyike Februari
16.
Kikao hicho kilikubaliana kuwa uchaguzi
ufanyike kwa katiba ya zamani kwani mchakato wa katiba mpya unaweza kuchukua
muda mrefu, hivyo kusababisha viongozi waliopo madarakani kuendelea kukalia
viti kinyume cha katiba, jambo ambalo si sahihi.
Kutokana na hali hiyo viongozi wapya
watakaochaguliwa moja ya kazi zao kubwa itakuwa kuifanyia marekebisho makubwa
katiba ya chama hicho ili iende na
wakati.
Pia kamati ya utendaji imeunda kamati ya
uchaguzi na kumteua mwenyekiti wa zamani wa Taswa ambaye kwa sasa ni Ofisa
Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, kuwa Mwenyekiti
wa Kamati ya Kusimamia Uchaguzi Mkuu wa TASWA, ambapo pia kutakuwa na wajumbe
wengine wanne.
Wajumbe hao ni katibu mkuu wa zamani wa
Taswa, Mwina Kaduguda, Peter Mwenda na wanahabari Isakwisa Mwaifuge na Mbonile
Burton.
Fomu za kuwania uongozi zitaanza
kutolewa Februari 10 hadi 14 mwaka huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment