Bodi ya Wakurugenzi ya Barcelona,
imeufuta mpango wa kujenga uwanja mpya na badala yake umeafika kuufanyia
marekebisho Uwanja wa Cam Nou kuwa mkubwa na wa kisasa zaidi.
Wakurugenzi hao wameipitisha propozo ya
kuuongeza uwanja huo kutoka kuwa na uwezo wa kubeba watu 98,000 hadi 105,000.
Imeelezwa pauni milioni 495 zitatumika
katika shughuli hiyo ambayo pamoja na kuuongeza uwanja huo kutakuwa na sehemu
ya paa litakaloziba mzunguko wote we uwanja na kuacha sehemu ndogo tu ya
katikati ya uwanja.
Rais wa Barcelona, Sandro Rosell
amesema kufanya yote hayo ni lengo la kuongeza kipato zaidi kutokana na mapato
yanayotokana na watazamaji.
CAMP NOU YA SASA KWA NJE |
0 COMMENTS:
Post a Comment