Manchester United imeambiwa itoe pauni
milioni 40 kama ina nia ya kweli kumnasa kiungo nyota wa Chelsea, Juan Mata.
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho naye
amesema milango iko wazi kwa Mata kama anataka kuondoka.
Mourinho ameonyesha imani kubwa kwa
William, Oscar na Eden Hazard kuliko Mata.
Mata naye amekuwa akihofia kukosa
nafasi katika kikosi cha Hispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia kama
ataendelea kubaki Chelsea.
Kwa upande wa Kocha wa Man United,
David Moyes, ameonyesha ana nia ya kumpata kiungo huyo mwenye uwezo mkubwa wa
kutengeneza nafasi.
Hapa chini ni namna Mata anavyoweza
kutengeneza nafasi nyingi zaidi ya wachezaji karibu wote wa Man United.
0 COMMENTS:
Post a Comment