Mzunguko
wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara unaanza
Jumamosi (Januari 26 mwaka huu) kwa mechi tano katika miji ya Bukoba, Dar es
Salaam, Tanga wakati mechi ya Tanzania Prisons na Ruvu Shooting inahamishiwa
uwanja mwingine.
Ashanti
United itacheza na Yanga kwenye Uwanja wa Taifa, Coastal Union itacheza na
Oljoro JKT katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga wakati Uwanja wa Azam Complex, Dar
es Salaam utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Azam na Mtibwa Sugar.
Jumapili (Januari
26 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya JKT Ruvu na Mgambo Shooting
itakayofanyika Uwanja wa Azam Complex wakati Simba na Rhino Rangers zitaumana
kwenye Uwanja wa Taifa.
Mechi ya
Tanzania Prisons na Ruvu Shooting iliyokuwa ichezwe Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sokoine inahamishiwa uwanja mwingine kwa vile huo bado nyazi zake ambazo
zimepangwa hivi karibuni hazijawa tayari kuhimili mechi hiyo.
Hivyo
Tanzania Prisons inatakiwa kutafuta uwanja mwingine unaokidhi viwango
vinavyotakiwa kwa ajili ya mechi hiyo, na nyingine dhidi ya JKT Ruvu
itakayochezwa Januari 29 mwaka huu.
Pia
matumizi ya tiketi za elektroniki yanaanza katika mzunguko huu kwa vile viwanja
nane ambavyo tayari vimefungwa vifaa vya tiketi hizo. Vilevile tunakumbusha
washabiki wa mpira wa miguu kuwa tiketi za elektroniki haziuzwi viwanjani.
0 COMMENTS:
Post a Comment