Wanachama wa Simba wamepinga maamuzi
yaliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) juu ya mwenyekiti wa klabu
hiyo Ismail Aden Rage.
Wakizungumza kwenye mkutano waliouandaa jana, wanachama hao kutoka sehemu mbalimbali nchini
walisema hawakutarajia kama TFF ingetoa maamuzi kama hayo kwa mwenyekiti wake
na kwamba walitegemea kuona shirikisho hilo lingesimamia kwa sheria na katiba
suala hilo lakini wamefanya ndivyo-sivyo.
Walisema wameshangazwa na hatua ya
kumtaka mwenyekiti huyo ajaze nafasi zilizoachwa wazi ikiwemo ya makamu
mwenyekiti ambayo kikatiba alitakiwa afanye hayo ndani ya siku 90 na mpaka sasa
zimefikia siku 270 bila kufanya lolote.
Kwa hali hiyo wamesema watamuandikia
barua Rage ya kumtaka aitishe mkutano wa dharura ambao lengo lao kubwa ni kujadili uvunjwaji wa katiba na marekebisho ya katiba mpya ya klabu hiyo na
nakala moja wataipeleka TFF.
“Hatukubaliani kabisa na maamuzi ya TFF
juu ya suala hili la Rage kumrejesha kama mwenyekiti na pia kumtaka kuchagua
makamu mpya wakati siku zimepita,” alisema
Makamu Mwenyekiti wa Tawi la New Mapambano Temeke-Mwisho mwenye kadi namba 087.
“Rage ni tatizo Simba tena ni kwa muda
mrefu, huyu kidume anatusumbua sana, tulijua TFF mpya ingesimamia kwa haki
suala hili lakini nayo imekosea, inaonekana kumbeba Rage ambaye anafanya mambo
mengi kienyeji, sijui wanamuogopa!” alisema mwanachama Hussein Mwaikamba wa
Iringa mwenye kadi namba 06563.
0 COMMENTS:
Post a Comment