Na Mwandishi Wetu
Kocha wa Simba, Zdravko Logarusic sasa
ndiyo chaguo la kwanza la Yanga katika nafasi ya kocha mpya iliyoachwa na Ernie
Brandts.
Taarifa za uhakika zinasema tayari Yanga
zimetuma mtu afanye mazungumzo na kocha huyo raia wa Croatia ambaye anaonekana
atawezana na mstaa wa Jangwani.
Mtoa habari ameliambia Championi
Jumatano jana mchana kuwa Yanga wamemtuma mtu huyo kufanya mazungumzo na
Logarusic.
“Mtu huyo ndiye atazungumza na kocha ili
kuangalia kama atakubali kutua Yanga, unajua ana mkataba wa miezi sita tu.
Hivyo pamoja na pilika za Yanga kutafuta kocha, lakini inaonekana chaguo namba
moja ni huyo wa Simba,” kilieleza chanzo.
Juzi, Logarusic alisema anauheshimu
mkataba wake wa miezi sita Simba ingawa hakukanusha au kukubali lakini jana
simu yake ilikuwa haipokelewi, wala hakuna ujumbe aliojibu pamoja na kuulizwa
maswali kadhaa na gazeti hili kama ameishamalizana na Jangwani.
Chaguo la pili la Yanga limeelezwa kuwa
ni Bobby Williamson anayefundisha Gor Mahia ya Kenya ambaye jana alizungumza na
Championi na kusisitiza.
“Mara zote nimesema wazungumze na
uongozi, mkataba wangu unaisha mwezi wa saba, kama watakuwa tayari kuniachia
sawa ila hapa nilipo nina furaha,” alisema.
Tayari uongozi wa Gor Mahia umeonyesha
hauna tatizo na umeikaribisha Yanga kuzungumza ili kupata mwafaka kuhusiana na
kocha huyo raia wa Scotland.
Sababu ttau kuu zinaonyesha tayari
Logarusic ametua Yanga mguu mmoja:
Mkataba:
Mkataba wake ni wa miezi sita tu na unamruhusu
kuondoka bila ya masharti kwa kuwa alikuwa chini ya uangalizi, hivyo inakuwa
lahisi zaidi kwa Yanga.
Mshahara:
Mshahara wake Simba ni dola 3,000,
wakati Brandts alikuwa anachota dola 11,000 katika mkataba wake mpya.
Hivyo ni lahisi kumshawishi kama atapewa
angalau hata mara mbili au tatu ya mshahara wake wa sasa Simba na akarukia
upande wa pili.
Viongozi:
Inaonekana viongozi Yanga wameshindwa
kujizuia, kuonyesha ‘mapendo’ kwake kutokana na uwezo aliouonyesha wa
kuibadilisha Simba ndani ya muda mfupi sana. Lakini alionyesha hahofii nyota
yoyote siku alipoichapa Yanga 3-1, maana alikuwa nabadilisha tu hata kama ni
nahodha.
Kwa waandishi wenye majungu we unaongoza... Hebu wakati mwingine weka pembeni mahaba yako kwa YANGA zungumzia uhalisia wa soka... Hata gazeti lenu la Champion leo asimilia 90 za habari ukurasa wa kwanza ni kuhusu YANGA... Kuchukua wachezaji wa SIMBA pamoja na Kocha na hata wakibadilisha Jezi zikawa nyekundu na nyeupe YANGA hawawezi kuendelea kwa mfumo huo... Washauri wawe na mipango ya maendeleo na si kuigilizia kwa SIMBA... Badala uchambue kwa kina kuhusu kwanini Yanga hamejitoa Kombe la Mapinduzi je sababu walizozitoa zina mashiko... hivi wangepeleka timu wasingepata chochote katika kujiandaa na michuano ya ligi na Club bingwa Afrika... Wewe uko busy na majungu ya UYANGA wako...Shame on you
ReplyDeleteYanga waache ushoga wasingoje watafuniwe na simba then wao waje kumeza tu.
ReplyDelete