Mabingwa wa Afrika, Al Ahly wameendelea
na mazoezi jijini Dar es Salaam huku kila kitu kikifanyika kwa uficho.
Tayari Ahly wamefanya mazoez mara mbili
jijini Upanga na wamekuwa hawaruhusu mtu yoyote kuingia na kushuhudia mazoezi
yao kwenye Sekondari ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) ya Upanga jijini Dar.
Lakini SALEHEJEMBE ilishuhudia wakifanya
mazoezi mepesi jana na wakarudia tena leo asubuhi huku msisitizo ikiwa ni
kusuia watu kuingia.
Kawaida Ahly imekuwa moja ya timu makini
sana wanapofikia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na muda mwingi
wamekuwa na hofu ya kuhujumiwa.
Mechi yao dhidi ya Yanga itakuwa
keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na inatarajiwa kuweka
rekodi ya watu kwa kuwa wamepania kuwaona Waarabu hao wakishindwa kwa kuwa
Yanga haijawahi kuwafunga tokea mwaka 1982.
0 COMMENTS:
Post a Comment