Pamoja na Yanga kuvunja rekodi na
kuichapa Mbeya City kwa bao 1-0, imeshindwa kurejea kileleni maana Azam FC
imezidi kung’ang’ania.
Azam FC nayo imeshinda mechi yake ya leo
kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kwa kuichapa Kagera Sugar mabao 4-0.
Kutokana na ushindi ushindi huo, Azam FC
imeendelea kubaki kileleni ikiwa na pointi 36 huku Yanga ikifikisha 35.
Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na Mganda, Bryan Umonyi mawili, Kelvin Friday na Jabir Aziz 'Stima'.
0 COMMENTS:
Post a Comment