Kikosi cha Barcelona kimeshakwea pipa kwenda Mancheste, England
kwa ajili ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya wenyeji wake Man City,
kesho.
Picha iliyotupiwa kwenye mtandao wa Instagram na kiungo Cesc Fabregas
imemuonyesha akiwa kwenye ndege.
Fabregas ameonekana akiwa na wachezaji wengine katika picha hiyo
ambao ni
Alex Song, Carles Puyol na Gerard Pique wakionyesha kuwa tayari
kwa ajili ya mechi hiyo ya ligi ya mabingwa hatua ya 16 bora.
Man City ndiyo tishio kwa upachikaji mabao kwa sasa, lakini
Barcelona nayo inaonyesha kuanza kurejea kwa kuwa mechi yake ya mwisho
iliitandika Rayo Vallecano mabao 6-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment