Baada ya
kufanikiwa kupiga ‘hat-trick’ (mabao matatu) ya pili mfululizo katika michuano
ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Komorozine ya Comoro, mshambuliaji wa
Yanga, Mrisho Ngassa, amebakiza bao moja kumfikia aliyekuwa mfugaji bora wa
mashindano hayo msimu uliopita.
Alexis
Youngouda Kada wa timu ya Coton Sport ya Cameroon, ndiye aliyeibuka mfungaji
bora katika michuano hiyo msimu uliopita kwa kuzifumania nyavu mara saba.
Mpaka sasa
Ngassa ameshazifumania nyavu mara sita katika mashindano hayo baada ya kushuka
dimbani mara mbili, hivyo amebakiza bao moja afikie rekodi ya Alexis.
Katika mchezo
wa kwanza uliofanyika jijini Dar es Salaam ambao Yanga ilishinda mabao 7-0,
mchezaji huyo alizifumania nyavu mara tatu.
Alifanya
hivyo tena juzi Jumamosi ambapo timu hiyo ilipambana na Komorozine katika mechi
ya marudiano iliyofanyika nchini Comoro ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa
mabao 5-2, matatu kati ya hayo yakifungwa na Ngassa
0 COMMENTS:
Post a Comment