Bekiwa pembeni na nahodha wa Simba,
Said Nassor ‘Chollo’, amemaliza dozi iliyomuweka nje ya uwanja kwa muda wa wiki
tatu na sasa ameanza mazoezi mepesi.
Chollo alikumbwa na tatizo la nyonga
alipokuwa mazoezini takriban wiki tatu na nusu zilizopita ambapo baada ya
vipimo, alipumzishwa kwa wiki tatu kwa ajili ya matibabu.
Ofisa
Habari wa Simba, Asha Muhaji, alisema wiki tatu za Chollo zimeisha jana na
baada ya kurudi hospitali na kuangaliwa, ilibainika tatizo lake limekwisha,
hivyo ameanza mazoezi mepesi.
Hata hivyo, Chollo atalazimika kwenda
kwenye Hospitali ya Doctor’s Plaza kila baada ya siku mbili ili kuangalia
maendeleo yake.
“Zile
wiki tatu za tiba na mapumziko za Chollo zimemalizika leo (jana), kwa hiyo amekwenda
hospitali iliyomtibu mara ya kwanza ya Doctors Plaza na ameambiwa aanze mazoezi
mepesi.
“Atalazimika kuangaliwa kila baada ya
siku mbili, kama atakuwa amepona kabisa na kupewa ruhusa na daktari wa timu
kuanza mazoezi, basi atajumuika na timu mapema iwezekanavyo kwa ajili ya
maandalizi ya mechi zijazo za ligi,” alisema Muhaji.








0 COMMENTS:
Post a Comment