February 12, 2014

KAZIMOTO KAZINI...
Kiungo Mtanzania nyota wa Al Markhiya inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Qatar, Mwinyi Kazimoto ameweka rekodi ya kucheza mechi 11 zote kwa dakika 90.


Kazimoto aliyetokea Simba na kujiunga na Al Markhiya, ameweka rekodi hiyo baada ya kupiga mechi hizo 11, kimahesabu, amepiga dakika 990.
Kutokana na mwendo huo, Kazimoto ameisaidia timu yake kushinda mechi tatu mfululizo na sasa iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 21.
KAZIMOTO AKIWA NA KIKOSI CHA AL MARKHIYA

Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Doha, Kazimoto alisema wakati ligi ya nchi hiyo inaendea ukingoni, ugumu umekuwa ukiongezeka.

“Mechi ya mwisho pia tumeshinda, tulicheza dhidi ya timu ambayo ni ngumu na inapewa hata nafasi ya kutwaa ubingwa.

“Kadiri ligi inavyosonga ukingoni, mambo yanazidi kuwa magumu kwa kuwa ushindani unaongezeka,” alisema.


Kazimoto ameaminika katika kikosi hicho licha ya kuwa na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani, ndiye amepewa dimba la juu, yaani namba nane.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic