Mshambuliaji Emmanuel Okwi amejiunga na
kambi ya Yanga mjini Bagamoyo.
Okwi ambaye usajili wake umesimamishwa
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ameanza mazoezi na wenzake.
Akizungumza na SALEHJEMBE leo jioni,
Okwi amesema ameanza mazoezi na wenzake baada ya kufanya pekee kwa zaidi ya
wiki.
“Nilikuwa nikifanya mazoezi peke yangu,
sasa nimeungana na wenzangu na tunafanya mazoezi pamoja,” alisema.
TFF imesimamisha usajili wake kwa madai
kwamba kuna kesi tatu za msingi ambazo ni Simba kuishitaki Etoile du Sahel
ikitaka kulipwa dola 300,000, Okwi kuishitaki timu hiyo na yenye pia
imemshitaki Fifa.
Okwi alikuwa jukwaani akiishuhudia Yanga
ikivunja mwisho wa msimu kwa kuifunga Mbeya City bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa
jijini Dar.
0 COMMENTS:
Post a Comment