Uongozi wa
klabu ya Lazio ya Italia umelazimika kutoa maelekezo kuhusiana na mchezaji wake
wa timu ya vijana kwamba umri wake ni mdogo.
Minara
anayetambulika kuwa na umri ya miaka 17, amezua gumzo huku wengi wakipinga
kutokana na muonekano wake.
Gazeti moja la
Senegal, limesema raia huyo wa Cameroon mwenye jina halisi la Joseph Marie
Minala ana miaka 41 na si 17 kama inavyoelezwa, hali iliyosababisha kutolewa
kwa ufafanuzi huo.
Imeelezwa kweli
Minara ana miaka 17 lakini alikulia katika mazingira magumu na kusababisha
vurugu.
Hali hiyo
imesababisha Minara afute akaunti zake katika mitandao ya kijamii ya Facebook
na Instagram na kubaki na Twitter tu.


















0 COMMENTS:
Post a Comment