Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic
amesema kamwe hawawezi kuidharau Mtibwa Sugar.
Logarusic ambaye yuko mjin Morogoro
tayari kwa mechi ya kesho ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar amesema
watacheza kwa kujituma na kusahau ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Oljoro.
“Mechi iliyopita si yetu, tunaangalia
mechi dhidi ya Mtibwa na hakuna atakayeidharau.
“Utakumbuka kabla ya kuanza mzunguko wa
pili nilitangaza pointi zitakazokuwa ngumu sana, niliitaja Mtibwa Sugar.
“Ni moja ya timu imara na tunatarajia
upinzani mkali sana,” alisema Logarusic.
Awali, Mtibwa Sugar ilicheza na Simba
mechi ya kirafiki na timu hiyo chini ya Mzalendo, Mecky Maxime ikailaza Simba
bao 1-0.
0 COMMENTS:
Post a Comment