February 22, 2014


Manchester United imeonyesha uhai tena baada ya kushinda mechi ya Ligi Kuu kwa mabo 2-0.

Robin van Persie ndiye alianza kufunga bao kwa mkwaju wa penalty baada ya Patrice Evra kuangushwa ndani ya 18.



Lakini Wayne Rooney ambaye ameingia mkataba mpya na Man United, akapiga bao la pili.
Bao hilo lilikuwa la kuvutia, kwani aliunganisha na mkwaju ukajaa kwenye kona ya lango.
Hali hiyo inaonyesha kuinua matumaini ya Wana Man United ambao wamekuwa hawana amani kutokana na timu yao kusuasua.
Kocha David ‘Daudi’ Moyes aliwaanzisha Marouane Fellaini na Adnan Januzaj ambao mara nyingi wamekuwa wakianzia benchi.
Mkongwe Rio Ferdinand pia aliongoza safu ya ulinzi ambayo imekuwa haiaminiki.






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic