February 23, 2014



Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amesema timu yake imepania kushinda mechi ya leo dhidi ya Ruvu JKT ili kuweka mambo sawa, lakini akakiri ushindi wa bao 7-0 wa Yanga dhidi ya Ruvu Shooting umewaongezea presha.


Simba inashuka dimbani leo Taifa kuivaa JKT inayoongozwa na kocha msaidizi wa zamani wa Yanga, Fred Felix Minziro ‘Majeshi’ au Baba Isaya.
Logarusic amesema leo lazima washinde katika mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa, Dar ili kufanya mambo yaende katika mwendo mzuri.
“Najua wengi watataka tuone tunashinda mabao mengi zaidi, lakini kikubwa kwetu cha kwanza kitakuwa ni pointi tatu.
“Kama litafuata suala la mabao mengi, basi hilo pia ni muhimu sana kwetu. Lakini pointi tatu tutazipa kipaumbele,” alisema.
Logarusic alikuwa katika uwanjani wakati Yanga ikiibutua Ruvu Shooting kwa mabao 7-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, jana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic