Kocha
Msaidizi wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa yuko
uwanjani akiishuhudia Al Ahly ikipambana na CS Sfaxien ya Tunisia.
Mechi hiyo ya
Kombe la Super Cup dhidi ya wababe hao wawili wa Afrika inapigwa muda huu kwenye
Uwanja wa Jeshi jijini Cairo na mashabiki 20,000 wameruhusiwa kuingia.
Mkwasa
amezungumza na SALEHJEMBE na kusema tayari ameanza kuishuhudia mechi hiyo.
“Niko
uwanjani naishuhudia mechi, mambo mengine tutazungumza. Hapa bado haijaanza
lakini baada ya muda mchache ujao timu zitaingia uwanjani,” alisema Mkwasa.
Yanga imemtuma
Mkwasa kwenda kuisoma Al Ahly kama ambavyo timu hiyo ya Misri ilivyofanya kwa
Yanga wakati ikicheza na Komorozine ya Comoro jijini Dar.
Yanga
itaivaa Al Ahly katika mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika Machi Mosi
jijini Dar na kurudiana jijini Cairo wiki moja baadaye.
Ndiyo maana
uongozi wa Yanga ukaona ni jambo la muhimu kumpeleka Mkwasa na blog hii ilikuwa
ya kwanza kueleza kuwa Yanga watatuma mtu Cairo.
0 COMMENTS:
Post a Comment