KWELI ushabiki wa soka ni hatari, mashabiki wa Simba na Yanga, juzi
almanusura watwangane makonde katika mazoezi ya Yanga yaliofanyika kwenye
Viwanja vya Tanganyika Packers jijini Dar, kisa kikiwa ni ubishani juu ya
usajili wa Emmanuel Okwi.
Katika mazoezi hayo, baadhi ya mashabiki walioonekana kuwa ni wa Simba
waliovalia jezi nyekundu, walifika uwanjani hapo na kukuta mazoezi yakiendelea,
ndipo wenzao wa Yanga wakaanzisha ubishi huo ambao ulizidi kukolea kadiri muda
ulivyosonga.
Ubishi huo uliongezeka kiasi cha kufikia pande zote kuanza kutishiana,
ambapo wa Yanga wengi walikuwa wakidai kuwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
limefanya makosa kumzuia kucheza huku wenzao wa Simba wakidai kuwa Okwi hana
uhalali wa kuichezea Yanga.
“Baba wa soka Fifa tayari ameshasema kuwa Okwi ni mchezaji halali wa
Yanga halafu anatokea kidudu mtu eti anasema mpaka ajiridhishe,” alisikika
shabiki mmoja wa Yanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment