CHANGA (WA TATU KUSHOTO MSTARI WA NYUMA) ALIPOKUWA AKIKIPIGA JKT RUVU. |
Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Omary Changa amefariki dunia
Taarifa hizo zimethibitishwa na baba
yake mzazi aliyejitambulisha kwa jina la Idd Changa.
“Ni kweli, tumepewa taarifa leo jioni
kwamba Omary aliokotwa kwenye eneo la Jangwani na mwili wake una kovu sehemu ya
usoni karibu na jicho.
“Bado hatujajua hasa tatizo nini na
kesho nimetakiwa kwenda Polisi ambako nitapata uhakika kwamba nini kilitokea
“Wengine wanasema alinyongwa, wengine
wanasema amepata ajali ya bodaboda, sasa tunakuwa hatuelewi hasa tatizo ni
nini?”
0 COMMENTS:
Post a Comment